Online Instagram Content ViewerImgGra
  1. Homepage
  2. itaendelea

#itaendelea photos and videos on Instagram

Medias attached with hashtag: #itaendelea on Instagram

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SIMULIZI:John and Nunu (KIONJOO) 07

MTUNZI:LAMECK PETER.  Matone Ya Damu Yaliweza Kudondoka Kwenye Barabara Na Maafande" - 1934064188092982004
ReportShareDownload023

SIMULIZI:John and Nunu (KIONJOO) 07 MTUNZI:LAMECK PETER. Matone Ya Damu Yaliweza Kudondoka Kwenye Barabara Na Maafande Waliligundua Hilo Na Kubwa Zaidi Waliweza Kugundua Yakuwa Mtu Huyu Alikuwa Kwenye Gari Iliyowazi Kwani Vitone Vile Vilikuwa Vikidondoka Kwa Umbali Kidogo.Polisi Walitoa Taarifa Sehemu Mbalimbali Juu Ya Utafutwaji Wa Jambazi Huyo Mkongwe Atafutwe.John Alianza Kutafutwa Kama Pesa.Gari Alilopanda John Lilifika Mahali Likatoka Kwenye Barabara Ya Lami Na Kuingia Kwenye Barabara Ya Vumbi.Kwa Inavyoonyesha Gari Hiyo Ilikuwa Ikielekea Shamba(Ushagoo).John Hakutaka Kupoteza Muda Aliamuwa Kujitoa Mwanga Kwa Kujirusha Kutoka Katika Gari Hilo Baada Ya Kuona Gari Hilo Limepunguza Mwendo.John Alipondoka Aliweza Kujivuta Vuta Iliaweze Kukaa Pembeni Kidogo Apumzike Kwani Alikuwa Amechoka Sana Na Damu Nyingi Zilikuwa Zime Mtoka.Aliketi Mahali Akijipumzisha.Wakati Akiwa Amejipumzisha Alijikutwa Akipatwa Na Usingizi Mzito Na Kupitiwa Na Usingizi Huo.Alipokuja Kuamka Alijikuta Akiwa Yupo Ndani Ya Nyumba Ya Manyasi Na Kitanda Cha Kamba Dalili Zilizo Onyesha Ni Mazingira Ya Kijijini.Muda Huo Ilikuwa Yapata Alfajiri Ya Saa Kumi Na Moja 11.Aliamuwa Kujivuta Vuta Na Kuketi Vyema.Muda Mchache Walikuja Vijana Wa Wili Pamoja Na Binti Mmoja Wakimweleza Yaliyotokea Na Yakwamba Walimuokota Na Wamempa Huduma Na Sasa Anatakiwa Kupumzika Kwanza.John Aliendelea Kupumzika.Asubuhi Na Mapema Palipokucha Saa 12 Asubuhi Na Mapema Aliamshwa Na Mabishano Yaliyokuwa Nje Hali Iliyomshtusha Sana. MWANAKIJIJI:Unae Mtafuta Hayupo Hapa. MTU:Nasemaje Yupo .Wewe Unacheza Na Akili Zetu Sio.Ghafla Mtu Yule Alipiga Risasi Juu Na Hakuwa Peke Yake Bali Walikuwa Kundi.Muda Mfupi Tu John Alishangaa Kuona Watu Hao Wakiingia Katika Chumba Alichokuwa Kumbe Walikuwa Ni Polisi.John Aliogopa Sana Na Matumaini Yake Yalipotea Ghafla.Mapolisi Wale Bila Huruma Wala Uoga Walimkamata Kama Vile Mtu Aliyemzima Tena Na Vipigo Juu.John Alilia Sana Tena Sana ,Alimkumbuka Sana Mpenzi Wake Nunu Aliyelala Kaburini Muda Huo. JOHN:Jamani Mimi Sijaua Mna Nionea Bure.Nioneeni Huruma Jamani Kwanini Lakini Mnanifanyia Hivi Na Mimi Ni Binadamu Kama Ninyi,Nimezaliwa Na Mama Ninaumia . #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SIMULIZI:John and Nunu (KIONJOO) 6.
MTUNZI:LAMECK PETER.

John Alishambuliwa Na Risasi Zilizokuwa Zikipigwa Na Jeshi La " at Dar es Salaam, Tanzania - 1934057776981949963

SIMULIZI:John and Nunu (KIONJOO) 6. MTUNZI:LAMECK PETER. John Alishambuliwa Na Risasi Zilizokuwa Zikipigwa Na Jeshi La Polisi Wakiwa Na Mke Wa Boss Odida.Polisi Walikuwa Wenye Kutoa Mashambulizi Kama Wako Vitani.John Aliporudi Ndani Kwa Haraka Haraka Mawazo Yake Yote Yalimtuma Aruke Ukuta.Japo Kuwa Hakujuwa Atakapo Ruka Ukuta Itakuwaje.Alimbidi Ajikaze Kiume.John Alichomoka Kama Risasi Akikimbia Kuruka Ukuta Ili Kuelekea Nje.Wakati Anakimbia Polisi Baadhi Walikuwa Wamekwisha Ingia Ndani.Wakati Anaruka Polisi Mmoja Alimtandika John Risasi Ya Kwenye Mguu.John Alipiga Kelele Za Maumivu Isivyo Kawaida Kwani Aliumia Na Hakuzoea Purukshani Hizo.John Alikuwa Akiwaza Mengi Akilini Mwake Kwani Hakuamini Kabisa Yanayo Mkuta.Aliporuka Huku Akiwa Ametandika Risasi Kwenye Mguu Mmoja Alibahatika Kuona Gari Ikipita Mbele Yake .Gari Iliyokuwa Imebeba Mizigo.Gari Ambayo Iliyokuwa Wazi Nyuma.John Aliruka Na Kuning'inia Kwenye Ile Gari Na Kuingia Ndani Ya Ile Gari Iliyofunikwa Na Turubai Ili Asipate Kuonekana.Kweli Mungu Mwacheni Aitwe Mungu.Gari Lile Lilipita Mbele Ya Polisi Hao Lakini Hawakugundua Kitu Hata Kidogo.Ukweli Ni Kwamba John Hakufanya Mauji Ila Ameweza Kuingizwa Katika Fungu La Wauaji Na Kuepuka Kesi Hiyo Kwasasa Itakuwa Ngumu Sana Kwake Kwani Hata Ameweza Kukimbia Na Huo Ni Ushahidi Ya Kwamba John Amefanya Mauji Japo Kuwa Hakufanya.Gari Lile Lilitembea Mwendo Kidogo John Akiwa Ndani Ya Gari Lile.John Hakuweza Kuruka Kwani Gari Lilikuwa Kwenye Mwendo Alitaka Kungojea Gari Lipunguze Mwendo Angalau Ndio Aruke Au Litakapofika Katika Barabara Ya Vumbi Aruke Kwani Atakapokaa Humo Hadi Mwisho Wa Safari Na Wakamkuta Humo Akiwa Katika Hali Hiyo Ya Jeraha Aliliyoshambuliwa Na Risasi Yatakuwa Ni Mengine Lakini Kingine Kibaya Zaidi Muda Mfupi Baada Ya Wao Kupita Pembezoni Mwa Polisi Wale Kumbe Jeraha Alilokuwa Nalo John Lilikuwa Likidondosha Damu Kwahiyo Walipopita Mahali Pale Matone Ya Damu Yaliweza Kudondoka Kwenye Barabara Na Maafande Waliligundua Hilo Na Kubwa Zaidi Waliweza Kugundua Yakuwa Mtu Huyu Alikuwa Kwenye Gari Iliyowazi Kwani Vitone Vile Vilikuwa Vikidondoka Kwa Umbali Kidogo #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SIMULIZI:John n Nunu (KIONJOO) 04
MTUNZI:LAMECK PETER.

John Alichomoka Kama Mshale Kwa Mwendo Wa Haraka Kisha Akamweka " at Dar es Salaam, Tanzania - 1933561700659226429

SIMULIZI:John n Nunu (KIONJOO) 04 MTUNZI:LAMECK PETER. John Alichomoka Kama Mshale Kwa Mwendo Wa Haraka Kisha Akamweka Nunu Kwenye Boksi Hilo La Kuwekea Mikate Hiyo.Alimpakia Haraka Haraka Huku Akitetemeka Na Huku Jasho Jingi Likimtiririka.Alimpakia Nakuanza Kumkokota Akitoka Nyumbani Hapo Akielekea Maeneo Ya Mbali Na Hapo Kwenda Kuutupa Mwili Huo.Wakati Anatoka Tu Anapiga Hatua Kama 20 Mke Wa Tajiri Odida Alitia Timu Nyumbani Hapo Akiwa Na Kikundi Cha Polisi Wa Sio Pungu Wa Tano.Walifika Nyumbani Hapo Wakiwa Na Mmoja Wa Wapangaji Aliyekuwa Akiishi Mahali Hapo Kumbe Alikwenda Kutoa Taarifa Kwa Boss Wake Na Nunu Baada Ya Kusikia John Akipiga Kelele Na Huku Akilitaja Jina La Nunu.Polisi Walifika Na Wakaingia Kwenye Vyumba Vya John Hawakupata Shida Kuingia Ndani Humo Kwani John Alisahau Kabisa Hata kufunga Mlango.Walipoingia Ndani Walikuta Baadhi Ya Michirizi Ya Damu Nzito Ya Binadamu Ikiwa Imetapakaa Ndani Humo.Walizidi Kutafuta Tafuta Ndani Humo Walikutana Na Ushahidi Mzito Wa Nguo Za Nunu Pamoja Na Nguo Nyingine Zake Na Mashuka Yakiwa Yameloa Damu Yakiwa Chooni Humo.Moja Kwa Moja Mapolisi Hao Waligundua Yakuwa John Amefanya Mauji.Walitoa Taarifa Kituoni Yakuwa John Atafutwe Tena Msako Mkali Kuanzia Sasahvi Anatafutwa Kwa Kesi Ya Mauji.Mke Wa Tajiri Odida Alijawa Na Majonzi Iliyoambatana Na Hasira Isiyo Ya Kawaida.Polisi Hao Walitoka Haraka Haraka Ili Kumtafuta John.Wakati Huo John Alikuwa Akiukokota Mwili Huo Akielekea Mbali Kidogo Ili Kwenda Kuutupa Mwili Huo.Akiwa Anakokota Mwili Huo Na Baiskeli Hiyo Itwayo Foneksi Alishangaa Kuona Gari Ya Polisi Iitwayo Difenda Ikipita Mbele Yake Kwa Kasi Ikionyesha Ya Kwamba Kuna Kitu Huko Kimetokea.John Aliogopa Sana Mapigo Yake Ya Moyo Yalidunda Mno Aliona Dunia Ni Mbaya.John Aliendelea Kung'ang'ana Na Zigo Lake Hilo Ili Akalitupe.Alikwenda Hadi Akafika Mahali Kulipokuwa Na Vichaka Vichaka Alilaza Baiskeli Ile Kisha Akajifanya Anakojoa Huku Akiwa Anaangalia Mazingira Kama Kuna Mtu Anamwona Au Anamtazama.Alipotazama Huku Na Huku Aligundua Yakuwa Hakuna Mtu Anaemwona Alifungua Boksi Lile Iliautoe Mwili Huo.Alipokuwa Akiutoa Mwili Huo Alishangaa Kuona Mbele Yake #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SIMULIZI:John and NuNu (KIONJOO) 03
MTUNZI:LAMECK PETER.

John Hakuamini Macho Yake Alianza Kumsukumiza Sukumiza Nunu La" at Dar es Salaam, Tanzania - 1933264170071335931

SIMULIZI:John and NuNu (KIONJOO) 03 MTUNZI:LAMECK PETER. John Hakuamini Macho Yake Alianza Kumsukumiza Sukumiza Nunu Lakini Nunu Hakuamka Wala Hakuonyesha Dalili Hata Za Kuamka.John Alichanganyiki Na Akili Zilimluka Alijikuta Akianza Kulia Na Kupiga Kelele.Lakini Baada Ya Kama Dakika Tano Aligundua Kuwa Jambo Hili Linaweza Kuja Kumsababishia Mambo Makubwa Sana Kwani Alijuwa Kabisa Tangu Nunu Alipoondoka Kwao Au Kwa Tajiri Wake.Tajiri Wake Atakuwa Amekwisha Anza Kumtafuta Na Anaweza Hata Akawasili Hapo Sio Muda.Aliamuwa Kujikaza Kiume,Alisimama Na Akachukuwa Kitambaa Na Maji Na Kuanza Kuzifuta Zile Damu .Alifuta Pale Chini Na Kuhakikisha Kuwa Mtu Anapoingia Mule Ndani Hagunduwi Kitu.Baada Ya Kupasafisha Mahali Hapo Na Huku Muda Ukizidi Kusogea Aliamuwa Kuvaa Nguo Haraka Haraka Ili Ajuwe Atafanya Ustaarabu. John Alikuwa Akiwaza Juu Ya Mwili Huo Alitafakari Sana Sana Lakini Mwisho Wake Aliamuwa Akautupe Mwili Huo.Aliufunga Tena Vizuri Mithili Ya Maiti Iliyofungwa Sanda.Baada Ya Hapo,John Alikuwa Ana Baiskeli Aina Ya Foneksi Baiskeli Aliyokuwa Anatumia Kubebea Mizigo.Kwa Muda Huo Baiskeli Yake Ilikuwa Nje .Ilikuwa Ina Boksi Kubwa La Kubebea Mikate Lililofungwa Na Mipira Vizuri Ipasavyo.Nadhani Wengi Mnalifahamu Vyema Boksi Hilo Ni Boksi Lilotengenezwa Kwa Mabati Lililokaa Mfano Wa Tranka Wanaloifadhiaga Nguo Wanafunzi Wa Bording Au Hostel.Alitafakari Jinsi Gani Atakavyoweza Kutoka Na Maiti Hiyo Kisha Akaipakie Katika Boksi Lile La Mikate Ili Apate Kuondoka Akautupe Mwili Huo.Hayo Yote Aliyokuwa Akitafakari Nakufanya Alikuwa Akifanya Kwa Majonzi Huku Akilia Kwani Hakuamini Kabisa Na Roho Ilimuuma Sana Kuona Mtu Aliyempenda Na Kupanga Nae Malengo Yakuja Kuwa Mama Wa Watoto Wake Akifa Mikononi Mwake.Alijaribu Kuchungulia Nje Ili Apate Kuangalia Usalama.Alipotizama Nje Alimwona Mpangaji Mwenzie Mmoja Aliyekuwepo Nje Akielekea Kuoga Bafuni.Alivuta Subira Kidogo Alipoingia Bafuni Tu Kuoga.John Alichomoka Kama Mshale Kwa Mwendo Wa Haraka Kisha Akamweka Nunu Kwenye Boksi Hilo La Kuwekea Mikate Hiyo. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "SIMULIZI: John and Nunu (KIONJOO) 02
MTUNZI:LAMECK PETER.

Kweli Bwana John Hakutaka Kupoteza Muda Wala Kupoteza Nafasi " at Dar es Salaam, Tanzania - 1933260966193323531

SIMULIZI: John and Nunu (KIONJOO) 02 MTUNZI:LAMECK PETER. Kweli Bwana John Hakutaka Kupoteza Muda Wala Kupoteza Nafasi Hiyo.Alianza Kumvua Nguo Nunu Taratibu Akiwa Anamvua Nguo Za Juu Taratibu Alijikuta Akimdondosha Kitandani Na Kuendelea Kumpapasa Kimahaba.Lakini Wakati Wanapapasana Kumbe John Tangu Alipoamka Hakuchomoa Neti Vyema.Neti Yake Ilikuwa Imeshikiliwa Na Mbao Mbili Zilizo Kuwa Mbele Na Nyuma Zenye Muundo Kama T " Nadhani Wengi Wengi Mnavijua Na Kama Hauvijuwi Kaulize Ili Upate Kujuwa"Wakati Anaendelea Kumpapasa Huku Akiwa Amesahau Kuchomoa Neti Hiyo.Walizidi Kulalia Neti Ile Na Ikaanza Kujivuta Taratibu. Mbao Moja Ya Mbele Ya Kitanda Kile Ilianza Kujivuta Kama Inataka Kudondoka Ikielekea Walipolala Akina John Na Nunu Lakini Kwa Muda Huo John Na Nunu Hawakuwa Na Habari Kabisa Walikuwa Wako Mbali Sana Kihisia.Wakiwa Wanaendelea Kulaliana Na Kupapasana Ghafla Mbao Ile Ilidondoka Na Kumwangukia Nunu Kwenye Upaji Wa Uso Ilipo Muangukia Iliweza Kumuangukia Nakumpiga Maeneo Ya Nyuma Ya Kwenye Kichogo Ghafla Kutokwa Na Damu Nyingi .Ghafla Mapenzi Yaligeuka Patashika John Ilimbidi Amwinue Nunu Aliyekuwa Juu Yake Ili Apate Kumsaidia Kwani Alikuwa Akitokwa Na Damu Nyingi Zilizo Tapakaa Kwenye T-shirt Yake Na Hata Kwenye Kitanda Chote.Muda Huo John Alikuwa Amekwisha Vua Nguo Zote Amebakiwa Na Boxer Na Kwa Upande Wa Nunu Alikuwa Amebakiwa Na Chupi.John Ilimbidi Amwinue Nunu Na Kumkalisha Chini.Muda Wote Huo Nunu Alikuwa Akilia... NUNU:John Mpenzi Wangu Mwenzio Nakufa Jaman.Alikuwa Akizungumza Katika Sauti Ya Chini Sana.Kauli Hizo Zilimchanganya Sana John Alijikuta Sasa Badala Ya Kumpa Huduma Anaanza Kumbembeleza. JOHN:Usiseme Ivyo Mbona Unazungumza Kauli Nzito Kama Hizo.Hauwezi Kufa Utapona Yaani Kiubao Hiki Ndio Kikuuwe Kweli.Muda Huo Wote Nunu Alikuwa Kitokwa Na Damu Sana ,Damu Zile Zilianza Kutapakaa Kwenye Sakafu.Muda Mchache Tu Ghafla Nunu Alinyamaza Kuzungumza.John Hakuamini Macho Yake Kumwona Mtu Aliyempenda Nunu Akifa Mikononi Tena Kwa Ajali Ndogo Tu Yakuangukiwa Na Ubao.John Hakuamini Macho Yake Alianza Kumsukumiza Sukumiza Nunu Lakini Nunu Hakuamka Wala Hakuonyesha Dalili Hata Za Kuamka. #itaendelea

Grandmaster (Stylish Kidd)👑 (@mr_celebrityy) Instagram Profile Photomr_celebrityy

Grandmaster (Stylish Kidd)👑

 image by Grandmaster (Stylish Kidd)👑 (@mr_celebrityy) with caption : "Video game stuff from @o.dembele7 
Dembele gool 👀

Dream Big! 😀🤙
📲follow @mr_celebrityy ❤️
Follow this  Account plz @mr_" - 1932248342919921487
ReportShareDownload037

Video game stuff from @o.dembele7 Dembele gool 👀 Dream Big! 😀🤙 📲follow @mr_celebrityy ❤️ Follow this Account plz @mr_celebrityy 👥tag friends👇 @neymarjr@mr_celebrityy 🚫IGNORE ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖               #itaendelea 🗽 Tag your friends

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 89 ‘Grace alifariki mwanangu pole sana babaa’ aliniambia
‘whaaaaat! ilikuajeee’" at Dar es Salaam, Tanzania - 1931865290750408787

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 89 ‘Grace alifariki mwanangu pole sana babaa’ aliniambia ‘whaaaaat! ilikuajeee’ nilimuuliza kwa mshangao sababu ya kutoamini alichokisema. ‘mwanangu Grace alifanikiwa kujifungua salama mtoto wa kike ambaye ndiye huyu hapa lakini baada ya kutoka hospitali na kurudi nyumbani kwenu kule mbezi beach alikutana na barua yako juu ya meza uliyomuandikia kuhusu kwenda kwako huko Oman kumtafuta Nairath kiukweli barua hiyo ndiyo ilikua chanzo kikubwa cha kifo chake kwani baada ya kuisoma tu presha ilimpanda akaanguka chini na kupoteza fahamu kitu kilichofanya arudi tena hospitali ambako alilazwa siku 3 na siku ya 4 saa 5 na nusu usiku akaaga dunia pasipo hata kumpa jina mtoto wake.’ mama aliniambia. ‘ni makosa yangu mama, kwa hiyo huyu ni mwanangu’ nilimuuliza. ‘ndiyo ni mwanao kabisa’ mama alinijibu. ‘mmempa jina gani?’ nilimuuliza tena. ‘tuliamua kumpa jina la Nairath kama ishara ya kuwakumbuka nyote’ alisema. ‘Nairaaaath!!?’ nilimuuliza kwa mshangao. ‘ndio anaitwa Nairath mbona umeshtuka’ aliniuliza huku nae akianza kulia. ‘mama Nairath nae amefariki na hawa hapa ni watoto wetu huyu wa kiume anaitwa Javier,na huyu wa kike anaitwa Grace’ Nilimwambia mama yangu huku nikizidi kulia na kumuelezea kila kitu na baada ya kumueleza aliwasogelea na kuwakumbatia huku na mimi kwa mara ya kwanza nikimnyanyua yule mtoto wangu na Grace na kumkumbatia kwa furaha na huzuni nyingi kwa sababu ya jina lake la Nairath kunikumbusha yale yote yaliyotokea kule Oman . baada ya hayo yote mama alitutarishia chakula nika kila na kukimaliza kisha nae kwa mara ya kwanza akaenda kuwaogesha wale wajukuu wake wawili nilioenda nao na kuwanywesha maziwa ya kopo aliyokua akiyatumia yule Nairath mdogo na ghafla akiwa katika kuwanywesha baba yangu mzee Hernandez aliingia ndani akiwa ametoka national stadium kuangalia mpira na baada ya kuingia tulisalimiana akawaona wajukuu wake wapya tukaongea mengi na kisha tukaenda kulala. Nilikuja kuamka majira ya saa 3 asubuhi kwa sababu ya uchovu, nikamsaidia mama yangu kuwaogesha wale watoto wangu #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 88
MTUNZI: FREDRICK LIBENA JAVIER HERNANDEZ ‘kila la heri sitokusahau’
‘mimi pi" at Dar es Salaam, Tanzania - 1931862027145714155

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 88 MTUNZI: FREDRICK LIBENA JAVIER HERNANDEZ ‘kila la heri sitokusahau’ ‘mimi pia sitokusahau kila la heri’ tuliagana. Ilikua ni huzuni kubwa sana katika kuagana kwetu ambapo baada ya kumaliza niliingia mpaka hotelini nikiwa pamoja na wale watoto wangu na nikaanza kupanga mizigo yangu pamoja na kile chumba nilichokikabidhi siku hiyo muda mchache kabla ya kwenda airport kuianza ile safari ya kurejea nyumbani nchini Tanzania. Nilienda mpaka airport pale Musqat mjini nikiwa pamoja na watoto wangu sote tukaingia ndani ya ndege ya Oman airways mali ya serikali hiyo na baada ya kuingia safari yetu ya kuelekea nyumbani nchini Tanzania ikaanza. licha ya ule urefu wa safari pamoja na usumbufu nilioupata kutoka kwa wale malaika wangu wadogo tulifanikiwa kufika na kutua salama juu ya kiwanja cha ndege cha mwl Julias Nyerere na bila kuchelewa nilichukua tax nikapakia mizigo yangu pamoja na wale watoto wangu na safari ya kuelekea nyumbani kwa wazazi wangu ikaanza huku hofu kubwa ikionekana kuuvaa mwili wangu kwa sababu ya kuogopa kupokea taarifa zozote mbaya za Grace pamoja na lawama zilizokua zikisubiri kunishambulia. Tulifika salama mpaka nyumbani kwa wazazi wangu na baada ya kufika kwa wasiwasi mwingi na hofu kubwa niliusogelea ule mlango wa kuingilia sebleni huku nikiwa nimewabeba watoto wangu pamoja na ile mizigo yangu. sikuamini kabisa nilichokiona mara tu baada ya mimi kuingia ndani. Nilimuona mama yangu mzazi akiwa anacheza na mtoto mdogo wa kike ambaye alionekana kufanana sana na Grace. ‘mama mwanao nimerudi naomba unisamehe sana mama’ nilisema huku nikilia na kuwashusha wale watoto wangu kisha nikapiga magoti na kumsogelea. ‘karibu sana mwanangu’ mama alinijibu huku akinikumbatia kwa furaha. ‘asante mama naomba unisamehe sana’ nilimwambia. ‘nisha kusamehe mwanangu’ alinijibu. ‘asante mama vipi Grace yuko wapi’ nilimuuliza kwa hofu kubwa kwa sababu ya kuogopa kunyeshewa mvua ya lawama. ‘Grace alifariki mwanangu pole sana babaa’ aliniambia ‘whaaaaat! ilikuajeee’ nilimuuliza kwa mshangao sababu ya kutoamini alichokisema. #itaendelea