Online Instagram Content ViewerImgGra
  1. Homepage
  2. burudanindomahalapake

#burudanindomahalapake hashtag

Posts attached with hashtag: #burudanindomahalapake

Evance Haule. (@mc_ejo) Instagram Profile Photomc_ejo

Evance Haule.

 image by Evance Haule. (@mc_ejo) with caption : "💥Ladies and gentleman 
Its moment to celebrate new couple in town
💕ALEX + OLIVER = LOVE ❤💖
Its perfect time to announce " - 1899708819376559970
ReportShareDownload044

💥Ladies and gentleman Its moment to celebrate new couple in town 💕ALEX + OLIVER = LOVE ❤💖 Its perfect time to announce that, they are OFFICIALLY Mr & Mrs ALEX GAMUYA #burudanindomahalapake

Evance Haule. (@mc_ejo) Instagram Profile Photomc_ejo

Evance Haule.

 image by Evance Haule. (@mc_ejo) with caption : "All the way from Ifakara
#AlexwedsOliver
#bethlehemhall
Vibe kama loteeeee.....
#watapatatabusana 
#shereheyenyeviwango " - 1899679919196008163
ReportShareDownload470

All the way from Ifakara Vibe kama loteeeee..... #burudanindomahalapake

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 32

Macho ya Frank yalimuangalia na kujilaumu moyoni kumtesa msichana mzuri kama huyo.
“pole Frank.” Alio" at Dar es Salaam, Tanzania - 1849092395189093824

MAPIGO YA MOYO 32 Macho ya Frank yalimuangalia na kujilaumu moyoni kumtesa msichana mzuri kama huyo. “pole Frank.” Aliongea Lulu baada ya kumuona Frank akimuangalia. “ahsante, nimeshapoa baada ya kukuona tu.” Aliongea Frank na mama yake akaamua kuondoka kwakua alijua kuwa maongezi yanayoendelea yalikuwa hayamuhusu. “jamani nini tena kimekupata?” aliongea Lulu na kuonyesha ishara za kujali. “ni mitihani tu ya dunia .” aliongea Frank na kumuangalia Lulu kwa macho ya haya. “pole, mungu atakujaalia tu utapona.” Aliongea Lulu kwa hali ya kumuonea huruma Frank. “Lulu, najua kuwa kwa sasa unaweza kuwaza kwa nini nimeamua kukuita. Kusema ukweli, yule msichana niliyekuambia kuwa ni chaguo la moyo wangu. Ndio aliyenisababishia yote haya. Nilipotea njia. Ila kwakua yameshanikuta makuu ndio namekukubuka na kuona thamani yako ikiwa juu ya maisha yangu yaliyobakia. Ni wazi kuwa nakupenda ingawaje nilihisi utakuwa unanibana na kutokuwa huru kuwa na wasichana wengine. Ila nakuapia kuwa hivi sasa najutia kwa kila nilichokutendea na naomba uupokee moyo wangu mkosefu mbele yako wewe uliyejaa uvumilivu na mapenzi ya kweli juu yangu. Nakutamkia kauli kutoka moyoni kuwa nahitaji msamaha wako ili niwe wako kwa mara nyingine.” Aliongea Frank maneno hayo huku machozi yakimtoka na kumfanya Lulu mwenye machozi ya karibu kuanza kulia na yeye. “Frank hakuna mwanaume duniani niliyeiweka rehani roho yangu kwake kama wewe. Ulinifunba macho na kuwa sioni kwa penzi lako. Ni wewe ndiye uliyenifundisha na kunionjesha matamu ya mapenzi. Na ni wewe pia ndio uliyeniingiza kwenye dimbwi la wanaolilia mapenzi na kuniumiza moyo zaidi ya nilivyoumia siku waliyokufa wazazi wangu. Kwanini Frank uliamua kunitenda?? Kwanini uliamua kuninyanyasa kwa maneno yaliyonifanya nitamani kuupoteza uhai wangu??? Kwanini ulinitamkia kuwa mimi si chaguo lako?? Kwanini Frenk??” Aliongea Lulu maneno hayo kwa uchungu na kumfanya machozi yaliashiria uchungu uliopo moyoni mwake kumwagika kama maji. Hali hiyo nayo ilizidi kumuumizi Frank na kumfanya nae azidi kulia kwa uchungu. Kila akisemacho Lulu kilikua cha ukweli. “naomba unisamehe Lulu. #burudanindomahalapake

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 30

Bila kuchelewa, wale wengine walianza kumpa kipigo cha haja Frank kwa magongo waliyonayo na wengine k" at Dar es Salaam, Tanzania - 1847753613281883422

MAPIGO YA MOYO 30 Bila kuchelewa, wale wengine walianza kumpa kipigo cha haja Frank kwa magongo waliyonayo na wengine kumcharanga sehemu kadhaa na mapanga. Dakika mbili tu zilitosha kumuacha Frank akiwa hoi pale chini. “ukome kufuata wake za watu.” Aliongea yule mwarabu na kuondoka na kundi lake huku Neila akiwa amemlalia asishuhudie tukio alilofanyiwa Frank. Kipigo walichompa Frank kilimfanya apoteze fahamu. Aliokotwa na wasamaria wema waliokuwa wakipita eneo hilo na kumpeleka hospitali. Taarifa za kuumizwa kwa mtoto wao wa pekee ziliwafikia wazazi wa Frank na kwenda mbio hospitali waliyoelekezwa kuwa Frank yupo. “vipi hali yake Dokta.” Aliuliza mama yake Frank baada ya kumuona daktari aliyekuwa ana muhudumia Frank. “hali sio nzuri sana. Kwakua amepigwa sana maeneo ya kichwani, ndio sababu itakayomfanya kuchelewa kupata fahamu.” Aliongea daktari na kuwaangalia wazazi wa Frank walioonyesha kuchanganyikiwa. “sasa baba unatusaidiaje?” aliongea mama yake Frank kinyonge “kina kipimo cha bodymass index ndio tunachoenda kumpima muda huu ili tujue mwili wake mzima umepata majeraha kiasi gani.” Aliongea Daktari na kuingia kwenye chumba alichotaka kuingia awali. Wazazi wa Frank walirudi kwenye benchi kusibiri majibu ya kipimo hicho. “mwanangu sijui kama atapona.” Aliongea mama yake Frank na kuanza kulia. “mmh mke wangu. Unajichulia ukifanya hivyo. Chamsingi ni kumuombea dua apone na kuwa mzima kama zamani.” Aliongea baba yake Frank na kumbembelea mkewe. Masaa manne baadae, Daktari aliwaita na kuwapa majibu wazazi wa Frank. “majibu yanasema kuwa amevunjika mbavu mbili za kushoto kutokana na kupigwa na kitu au vitu vizito. Kubwa zaidi ni kuwa damu imevuja kwenye fuvu lake la kichwa. Cha kuchukuru mungu ni kwamba damu hiyo haijachanganyika na ubongo. Maana ingekuwa hivyo tungekuwa tunaongelea habari nyingine hapa. Nimewaita ili msaini kama mnakubali mtoto wenu afanyiwe operation kubwa ya kichwa ili tunusuru maisha yake.” Aliongea Daktari na kumfanya mama yake Frank kuanza kulia. Baba yake Frank aliamua kuanguka saini yake na Frank akapelekwa kwenye chumba maalumu cha kufanyia upasuaji. #burudanindomahalapake

makame 🔴 (@makame_symon) Instagram Profile Photomakame_symon

makame 🔴

ReportShareDownload011

tupate #burudanindomahalapake tbt 2005 io👀👀🇯🇲

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 19

Walitafuta jina la Neila na baada ya kumuona alicheka.
“sio mbaya lakini, ameshika nafasi ya 6.” Alio" at Dar es Salaam, Tanzania - 1841535295751567754

MAPIGO YA MOYO 19 Walitafuta jina la Neila na baada ya kumuona alicheka. “sio mbaya lakini, ameshika nafasi ya 6.” Aliongea kwa Dharau baada ya kuona kampita masomo yote tena kwa point nyingi. “hongera, umekuwa mtu wa 6.” Aliongea Frank baada ya kumuona Neila amejiinamia. Neila alinyanyuka akiwa na sura nyingine tofauti na ile aliyoizoea. Hali iliyomfanya Frank ashangae. “ hapa shuleni kila mtu ameletwa na mzazi wake, so matokeo yangu hayakuhusu. Ni nani amekuambia alikua anahitaji umuangalizie matokeo yake?.. kuongoza mitihani isiwe shida kwa wengine. Siku nyingi sana nilikua siipendi tabia yako ya kujisikia ndio maana nikakwambia ufute yako. Nikafikiri umejirekebisha kumbe ndio tabia uliyozaliwa nayo. Unafikiri sijakusikia ulipokuwa unajitamba eti nilifikiri nimepata mpinzani kumbe yule dada boya tu… acha shobo mtotoo wa kiume, fuata yako halafu tusijuane coz tumekutana chuoni tu hapa.” Maneno yale ambayo yalisika na umati mkubwa waliokuwa pale kutokana na Neila kuongea kwa nguvu, ndio kulikomfanya aumie sana rahoni na kupata aibu kubwa. Furaha yote aliyokuwa nayo juu ya kufaulu vizuri iliyeyuka kama barafu kwenye jua kali. Aliulaumu sana mdomo wake kwa kuropoka mambo ambayo yangemshusha maksi kwa Neila. Tukio hilo lilimkosesha raha Frank. Hakupenda kumchukiza Neila hata kidogo. Alijua kuwa kumuuzi binti huyo ni sawa na kujipa adhabu kali inayomuumiza mwenyewe. Urafiki ukafa kinamna hiyo. Hakukua na salamu wala maongezi yoyote kati yao. Awapo Frank sehemu yoyote, basi Neila hakusogeza miguu yake pale. Na hata kama Neila alikua anapiga story na watu mbali mbali, basi akija tu Frank yeye huondoka eneo hilo. Unyonge mkubwa ulimpata Frank na kujiona kuna kitu anakosa kutoka katika maisha yake. Alijiridhisha kwa kuwachukua marafiki wa karibu wa Neila na kutembea nao. Hiyo ndio ilizidi kumpunguzia maksi Frank na kuzidi kuchukiwa na Neila. Uwezo wake wa kusakata kabumbu ulipungua kiwango siku hadi siku. Kuna wakati hakua msaada kabisa kwa timu yao ya chuo. Kocha wao alimuita na kumuuliza ni nini tatizo. #burudanindomahalapake

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Habar wapenzi wa simulizi kwa hakika nafurahi kwa uwepo na support yenu. Hivyo bhasi nikiungana na @roryatv nimeamua kuwaletea kipindi cha simulizi zetu ambacho nitakuwa nikiwapatia simulizi tamu za kusisimua,kuburudisha na kuelimisha kwa simulizi za Mapenzi, maisha na uchawi... UNAANZAJE KUPITWA SUBSCRIBE OUR YOUTUBE CHANNEL LINK ON MY BIO N @roryatv #BURUDANINDOMAHALAPAKE